Jifunze Keyboard

Ili kuweza kupiga muziki kwenye keyboard, unahitaji kujua  namna ya kubonyeza button/vitufe mbalimbali kwenye keyboard yako ili kupata milio inayovutia. Zipo kanuni mbalimbali zinazoongoza ubonyezaji wa buttons hizo. Kanuni hizo zimepewa majina ya kitaalamu kama vile "Scale" na  "Chords". Zipo scales za aina nyingi na vilevile chords pia kama Major Chords, Minor, Seventh, Nineth, Major Seventh, Diminished, Augumented, Sixth, Fifth, Suspended Four, Suspended Two, Minor Nineth, Minor Seventh......na nyingine nyingi sana! Kwa kuanza tutajifunza namna ya kubonyeza kodi za msingi (Major Chords) kwa njia ya picha na kisha Major scale pamoja na vionjo kidogo vya "Blue scale".

Kuna jumla ya Major chords 12 (Kwa button nyeupe 7 na nyeusi 5)
Namna ya kushika/bonyeza Major chords ni kama inavyooneshwa kwenye picha hapo chini;

C Major (Bonyeza button za C, E na G)















D Major (Bonyeza D, F# na A)















E Major (Bonyeza E, G# na B)















F Major (Bonyeza F, A na C)















G Major (Bonyeza G, B na D)















A Major (Bonyeza A, C# na E)















B Major (Bonyeza B, D# na F#)














Note: # inasimama badala ya "Sharp" na b badala ya "Flat"

Kwa mafunzo zaidi na mifano kwenye nyimbo mbalimbali tafadhali nunua DVD yetu ya ''JIFUNZE KEYBOARD''- Beginner to Intermediate: ili uinue zaidi kiwango chako cha muziki.


LESSON NO. 2

WAYS TO BOOST AND IMPROVE YOUR KEYBOARD PLAYING:

There are several ways to improve the quality of your playing. Zifuatazo ni baadhi tu ya siri nyingi za kuboresha kiwango chako cha upigaji wa muziki katika muda mfupi;

1) Inversions
2) Chord Additions
3) Chord Omissions
4) Chord Suspensions
5) Chord Arpeggios
6) Chord Extensions
7) Chord Reaches
8) Chord Dissonance
9) Chord Substitutions
10) Polychord voicings
11) Grace notes

Nyingi kati ya 'siri' hizi nimezielezea kwenye DVD ya mafunzo ya muziki (JIFUNZE KEYBOARD Vol.1) hata hivyo twaweza kushea japo kwa maandishi tu hapa!


CHORD INVERSIONS:

Si wanamuziki wengi wanaotilia maanani au kufahamu siri kubwa iliyopo kwenye inversion katika kuboresha uzuri wa upigaji wao wa keyboard. Kwa haraharaka inversions zaweza kuonekana ni jambo dogo tu ambalo si la msingi sana lakini lina nguvu kubwa katika kuleta picha ya tofauti kabisa unakuwa makini katika matumizi yake. Kwa definition
“INVERSIONS are just different ways to play the same chord.”
Basically, every note gets its turn on the bottom. If you remember that, you’ll never forget how inversions work.
Kwa mfano kama tungetumia namba zifuatazo:
1 3 5 7
Na ikiwa tutatakiwa kuzipanga namba hizi kwa namna tofautitofauti huku kila mojawapo ikipata nafasi ya kuwa mwanzoni then ingeonekana kama hivi;
1 3 5 7
3 5 7 1
5 7 1 3
7 1 3 5
Sasa, kwa mtindo huohuo fikiria notes, zingeonekana hivi:
C E G B
E G B C
G B C E
B C E G
There you have it! You’ve mastered the “inversions” game.
So when you’re playing a particular chord and you think it can sound better, the first thing to do is try different inversions.
After hitting a chord, you can even follow up with other inversions of the same chord up your piano. Kwa njia hii peke yake inaweza kubadilisha kabisa upigaji wako wa muziki. Fanya mazoezi kwa chord zote unazozifahamu kuzipiga katika inversions na usikilize mabadiliko yake. Waweza kutumia inversion sasa kwenye nyimbo ambazo umekuwa ukizipiga the normal way. Mwanzoni waweza kupata ugumu katika kuzishika kutokana na kuzoea upigaji chords wa namna moja kwa muda mrefu ila baada ya mazoezi utazoea na kufurahia upigaji wako mpya!!!